3. Kula mafuta yenye afya zaidi.
Mafuta yenye afya, kama yale yanayopatikana kwenye mafuta ya mimea na samaki, yanaweza kuongeza mwitikio wa kinga ya mwili wako kwa vimelea kwa kupunguza vichocheo mwilini.
Ingawa uchochezi wa kiwango cha chini ni jibu la kawaida kwa mafadhaiko/mkazo/msongo wa mawazo au kuumia, uchochezi sugu unaweza kukandamiza mfumo wako wa kinga.
Mafuta ya mizeituni, ambayo ni ya kupambana na uchochezi sana, yanahusishwa na kupungua kwa hatari ya magonjwa sugu kama ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa kisukari cha aina ya pili. Pamoja, sifa zake za kuzuia uchochezi zinaweza kusaidia mwili wako kupambana na bakteria na virusi hatari vinavyosababisha magonjwa.

4. Kula vyakula vyenye chachu zaidi au chukua kirutubisho cha probiotic.
Vyakula vyenye uchachu(mfano Mtindi) vina utajiri katika bakteria wenye faida vinavyoitwa probiotic, bakteria ambao huishi katika njia yako ya kumengenya chakula.
Vyakula hivi ni pamoja na mtindi, sauerkraut, kimchi, kefir, na natto.
Utafiti unaonyesha kuwa mtandao unaostawi wa bakteria wa utumbo unaweza kusaidia seli zako za kinga kutofautisha kati ya seli za kawaida, zenye afya na viumbe hatari vya uvamizi.
Katika utafiti wa miezi 3 kwa watoto 126, nusu yao waliokunywa ounces 2.4 (mililita 70) ya maziwa yaliyotiwa chachu kila siku walikuwa na magonjwa ya kuambukiza machache karibu 20%, ikilinganishwa na ambao hawakunywa maziwa hayo (80%).
Ikiwa hauli chakula kama mtindi (fermented foods) mara kwa mara, virutubisho vya probiotic ni chaguo jingine jepesi kwako.

5. Punguza sukari iliyoongezwa.
Kulingana na utafiti wa uchunguzi kwa karibu watu 1,000, watu walio nenepa sana ambao walipewa chanjo ya homa walikuwa na uwezekano mara mbili wa kupata homa kuliko watu wasio na tatizo hilo ambao walipata chanjo.
Kwa kuzingatia kuwa unene kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari wa aina ya 2, na ugonjwa wa moyo vyote hivi vnaweza kudhoofisha kinga yako ya mwili. Kupunguza sukari iliyoongezwa ni sehemu muhimu ya lishe ya kuongeza kinga.
Unapaswa kujitahidi kupunguza ulaji wako wa sukari kwa chini ya 5% ya kalori zako za kila siku. Hii ni sawa na vijiko 2 vya sukari (gramu 25) kwa mtu aliye kwenye lishe ya kalori 2,000.

0 Comments