Mara nyingi tunahisi watu wenye afya hutopatwa na magonjwa au hawapati shida kubwa ya afya, uzito mkubwa, na kila wakati huwa na maisha yenye afya. 

Lakini je! Sisi ni wazima wa afya?

Ili kujua ikiwa sisi ni wazima wa afya, haikuchukui mda mrefu kusikiliza maoni ya wataalam wa afya. Viwango vya kiafya vinaonekanaje?

Hapa kuna ishara za mwili wenye afya kama ilivyo nukuu kutoka kwenye Orodha.

1. Nywele nene na Imara.

Nywele nyembamba, zenye matawi, kavu zinaweza kuwa alama ya shida za kiafya, kama vile hitilafu ya tezi, mafadhaiko/mkazo, na utapiamlo. Kinyume chake, nywele zenye afya pia ni kiashiria cha afya ya mwili.



2. Kucha Ngumu/Imara.

Dirisha lingine kwa afya ya mtu binafsi iko kwenye kila kidole, haswa kucha. "Kucha ni onyesho kamili la afya. Zaidi ya kile kinachotokea kwa kucha inajumuisha shida za mfumo au ngozi."


Kulingana na utafiti wa daktari, mkazo unaweza kuathiri kucha, nywele, na ishara kutokana na shida ya mwili wote. Kwa mfano, rangi nyekundu ya kucha na njano, na kucha za kukatika. Mbali na fangasi, hali hiyo inaweza kuwa ishara ya jipu/uchafu katika damu au upungufu wa damu.


3. Meno na Fizi Imara.

Afya ya mdomo pia ni kipimo cha afya. Meno yenye nguvu na ufizi wa pink ni kiashiria cha afya kwa mwili. Kama maeneo mengine ya mwili, mdomo ni kiota/makazi ya bakteria, ingawa nyingi hazina madhara. Lakini ikiwa usafi wa mdomo hautasimamiwa, bakteria inaweza kuwa hatari kwa sababu inaweza kusababisha maambukizo ya mdomo, meno kutoboka/kusagika, na ugonjwa wa fizi.



4. Mwili wenye Usawa wa Urefu na Uzito.

Kiini cha uzito wa mwili (BMI), ni kipimo cha uzito na urefu na vile vile kuwa kiashiria wakati kuna mafuta mengi mwilini. Watu ambao BMI ni chini au zaidi ya nambari iliyowekwa wanaweza kupata shida za mifumo ya mwili.



5. Kupata Usingizi wa kutosha.

Lazima tujue kuwa kunyimwa usingizi ni mbaya kwa afya na kunaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari, kuongezeka uzito, na magonjwa ya moyo.



6. Ushirikiano katika Jamii.

Matokeo ya uchunguzi yalisema ya kuwa; kuwa na marafiki wengi, kupata msaada kutoka kwa mitandao ya kijamii, na mwingiliano na wengine ni nzuri sana kwa afya, sio afya ya akili tu, bali pia ya mwili.



7. Lishe Bora.

Matumizi ya matunda na mboga za majani kila wakati kunaweza kupunguza shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na hatari ya kiharusi, kuzuia aina kadhaa za saratani, kupunguza hatari ya shida ya macho na mfumo wa chakula, pamoja na kudumisha  viwango vya sukari katika damu.