Umbo la mwili wako hausaidia kuamua nguo ambazo utaonekana bora zaidi, kupendeza zaidi, pia linaweza kuonyesha habari muhimu kuhusu afya yako. Tambua nini sura/muonekano wa mwili wako unamaanisha.

Ukiwa unaongezeka uzito wa ziada inategemea sababu nyingi kama maumbile ya kurithi, ushawishi wa homoni na aina ya maisha yako kama vile lishe, mazoezi na msongo wa mawazo. Ukiweza kutambua umbo la mwili wako, unaweza kutambua masuala ya kiafya ambayo yana uwezekano wa kukuathiri na kwa hivyo kuchukua hatua za kuzuia ama kupunguza athari za kiafya.
                                 

UKO KATIKA UMBO GANI?

Unaweza kutambua umbo la mwili wako kwa kutumia uwiano wa kiuno-kwa-hips/makalio (WHR). Ili kujua hili, gawanya vipimo vya kiuno chako kwa vipimo vya makalio/hips zako.

Kuamua mzunguko wa kiuno chako, pima sehemu ndogo/nyembamba kabisa ya kiuno chako. Kwa mzunguko wako wa hips, pima sehemu kubwa zaidi ya makalio yako. Gawanya kipimo cha kiuno kwa kipimo cha hips kupata uwiano wako wa kiuno-kwa-hips/makalio (WHR).
                                



Apple/Tufaha - WHR zaidiya 0.8 kwa wanawake, zaidi ya 0.9 kwa wanaume
Pear/Peazi - WHR chini ya 0.8 kwa wanawake, chini ya 0.9 kwa wanaume
 
                              

Wacha tuangalie kile kila umbo la mwili wako linaeleza juu ya afya yako.


UMBO LA TUFAHA

Ikiwa unalo "umbo la tufaha", uzito wako hujilimbikiza maeneo ya kiuno, hips na tumbo. Unakua mpana juu juu lakini mwembamba/mdogo chini. Wakati mwingine unaweza kuhisi miguu yako inaonekana kama ya mtu mwembamba zaidi.

Muonekano wa tufaha una uwezekano mkubwa wa kutokea kwa kuendana na umri mkubwa/uzee. Wanaume wana uwezekano mkubwa wa kuwa na umbo hili, hivo kuwafanya kuwa na "Kitambi/tumbo la bia".

Kwa jinsia zote, umbo hili la mwili linaonyesha ukosefu wa uwiano wa maisha kama vile kiwango cha juu cha mfadhaiko/msongo wa mawazo, lishe duni na mazoezi kidogo sana ya mwili. Kwa wanaume haswa, unywaji mwingi wa pombe umehusishwa na maendeleo ya umbo la tufaha.



AFYA:

Kwa miaka, madaktari wametambua uhusiano kati ya mlundikano wa mafuta kwenye eneo la tumbo na kuongezeka kwa athari za kiafya. Mafuta ya ziada katika eneo lako la katikati ya mwili, hukaa sio tu chini ya ngozi yako. Uchunguzi umeonyesha kuwa mafuta hujipenyeza zaidi katika viungo (organ) na yamehusishwa na hatari kubwa ya ugonjwa wa saratani ya utumbo na saratani ya matiti.

Mafuta hayo huingia ndani ya damu na huzunguka mwili mzima. Kuzidi kwa mafuta kama hayo kwenye mtiririko wa damu kunaweza kusababisha shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na mishipa na kisukari cha aina II.

Kwa mfano, utafiti ulifanywa kuangalia afya za wanaume na wanawake 200 wenye kisukari bila ugonjwa wa moyo. Ilionyesha kuwa umbo la tufaha na kitambi bila kujali uzito wa jumla wa mwili, linaweza kutabiri vizuri kufeli (ufanisi mbovu wa) kwa Ventriko (chemba ya moyo) ya kushoto, ambayo huleta madhara ya kujaa majimaji/giligili katika moyo na mapafu.

Zaidi ya hayo, utafiti umeonyesha kuwa usambaaji wa mafuta katikati ya mwili unahusiana na hatari kubwa ya kisaikolojia ya kufadhaika (msongo wa mawazo).

Ingawa haya yote yanaweza kuwa ya kuogopesha, mafuta huondoka kwa wingi mwilini kupitia kufanya mazoezi na kupata lishe yenye afya. Kwa hivyo ikiwa unafanya mazoezi kwa bidii, uzito unaweza kupotea na hatari za kiafya hupunguzwa.

AINA YA MAISHA:

Maisha ya kufanya mazoezi ni muhimu sana ikiwa una umbo la tufaha. Mazoezi aina ya Cardio na uzito hupendekezwa sana. Kuogelea, kuendesha baiskeli, jogging au mazoezi ya uzito yatasaidia kuweka asilimia ya mafuta ya mwili wako katika kiwango cha kawaida na chenye afya. 

Ikiwa una kazi ya ofisini (kukaa mda mrefu) na huwezi kupata wakati wa mazoezi, hakikisha kuinuka mara nyingi kunyoosha na kwenda kutembea kwa miguu wakati wa chakula cha mchana. Tumia ngazi kila wakati!

VYAKULA:

Watu wenye umbo la tufaha watafaidika na lishe iliyo na protini na nyuzi (fiber) nyingi na kiwango cha chini katika wanga. Hii itasaidia kudhibiti kiasi cha mafuta yaliyohifadhiwa kwenye mwili na vile vile mafuta yanayojaa katika mtiririko wa damu kuondolewa. Chagua matunda na mboga za majani pia epuka vyakula vya kusindika kama mkate mweupe na keki. 

Ongeza viungo zaidi kwenye milo yako kama vitunguu au pilipili kwani hizi huchochea kimetaboliki (utengenezaji wa nishati mwilini - mafuta kuunguzwa) na kuboresha kazi ya ini. Watu wenye umbo la tufaha wanakabiliwa na hamu ya kula baada ya chakula cha mchana, hivyo kuwa na vitafunwa vyenye afya tayari kujiepusha na kula vyakula vya mafuta.


UMBO LA PEMBE TATU:

Watu wenye maumbo ya mwili wa pembe tatu wana mabega mapana lakini viuno vyembamba na labda wanaonekana wa mazoezi/riadha sana.


AFYA:

Hili ni umbo zuri la kuwa nalo! Kwa sehemu kubwa ya misuli na urefu mzuri kwa uwiano wa uzito, umbo la pembetatu lina umetaboli (uunguzaji mafuta kutengeneza nishati) mkubwa. Watu ambao wana mwili huu hawapati uzito utokanao na mafuta kwa urahisi, na pia wakati wa kufanya Diet, wanafanikiwa zaidi katika kupunguza uzito.

Walakini, ikiwa watu wenye umbo hili hula lishe iliyojaa mafuta, wana uwezekano mkubwa wa kukutwa na ugonjwa wa moyo. Kwa kuongezea hiyo, watu ambao umbo la mwili wao linakaa katika kipengele hiki wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa mifupa (
osteoporosis).

MAZOEZI:

Lengo lako katika mazoezi inapaswa kuwa ni kujenga nusu yako ya chini - haswa mapaja yako na makalio - na kukitambua kiuno chako. Kupanda na kushuka ngazi, kichurachura vinaweza kuimarisha na kujenga mwili wako wa chini na kati. Kuchanganya hayo mazoezi na ya Cardio ya kiwango cha juu huweza kuondoa kabisa mafuta karibu na eneo la kati.

LISHE:

Ili kupunguza hatari za kiafya, wale walio na umbo la pembetatu geuzwa wanapaswa kutumia protini nyingi kutoka kwa vyakula kama kuku na samaki.