UMBO LA PEAZI:

Ikiwa wewe ni aina ya peazi, una umbo kinyume na lile la tufaha. Badala ya kuwa mzito na mkubwa juu, sehemu yako ya kiuno inakuwa pana kuliko mwili wako wa juu, na mafuta mengi yanalimbikizwa katika mapaja yako, kiuno na eneo la makalio.

AFYA:

Habari njema ni kuwa uzito ulio  katika umbo lako la chini na mapaja yako ni kwa sababu ya mafuta yaliyo chini au katika ngozi badala ya aina hatari zaidi yanayoingia ndani na katika mishipa ya damu. Watu wenye umbo hili wana afya bora zaidi kuliko wale walio na miili ya umbo la tufaha. 

Mafuta yaliyowekwa kwenye viuno hayana uwezo mkubwa wa kuzunguka mwilini, hivo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. Kwa kuongezea, hatari ya kiharusi na ugonjwa wa sukari haiko juu (sio kubwa) kwa watu wa umbo la peazi.

Walakini kuongeza uzito wa ziada kwenye viuno kunaweza kusababisha hatari kubwa ya ugonjwa wa mgongo (
osteoarthritis), na mafuta yana uwezekano mkubwa wa kuonekana kama cellulite.


Utafiti wa kisayansi umeonyesha pia kuwa maumbo ya mwili wa peazi yanaweza kupata ugumu zaidi kupunguza uzito kuliko yale ya umbo la tufaha. Hii ni kwa sababu mafuta kwenye mwili wa juu, kifua na tumbo huhamasishwa na mwili kutumika kuzalisha nishati zaidi kuliko mafuta yaliyo hifadhiwa chini, katika makalio, viuno na mapaja. 

Hii inamaanisha kuwa unaweza kulazimika kufanya bidii zaidi katika mazoezi ili kupunguza uzito kuliko rafiki yako aliye na mwili ulio na umbo la tufaha. Kwa sababu hii, ni muhimu sana kuwa watu wenye umbo la peazi kufuatilia kwa karibu ulaji wa mafuta na kupunguza matumizi ya mafuta.

Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kukusanya uzito/mafuta karibu na nusu ya chini ya miili yao kuliko wanaume, na wana uwezekano wa kuwa na viwango vya juu vya estrogeni, ambayo inaweza kuongeza hatari ya hali kubwa ya estrogeni kama saratani ya matiti. Kwa hivyo ni muhimu sana kwa wanawake wenye umbo la peazi kuangalia, kuchunguza ama kupima matiti yao kila mwezi.

MAZOEZI:

Fanya mazoezi ambayo yanalenga misuli ya mguu kama kukimbia au kutembea kwa nguvu na mafunzo ya nguvu. Kwa kubadilisha mafuta kuwa misuli, watu wenye umbo la peazi wanaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari yao ya kupata magonjwa.

LISHE:

Chagua vyakula vyenye protini nyingi na nyama isiyo sindikwa. Watu wenye umbo la peazi wanaweza kuwa na tabia ya kukasirika ama kupata mihemko kwa urahisi, hivyo hakikisha hauruki/huachi kula (milo). Kula mara kwa mara itasaidia kuleta uwiano katika viwango vyako vya sukari ya damu na mihemko/hisia.


UMBO LA MSTATILI:

Umbo la mwili la mstatili pia linajulikana kama rula, ndizi au mwili ulio nyooka. Watu wenye umbo mstatili huwa na uzito sawasawa juu na chini, lakini pia huweza ongeza uzito kuzunguka katikati yao (tumbo/kitambi).

AFYA:

Watu wenye umbo la mstatili huwa na kimetaboliki ya hali ya juu na hawazidi uzito kirahisi ikilinganishwa na maumbo mengine. Kwa hivyo wanaweza kula vyakula vingi kwa wastani. Jambo la muhimu ni kuweka umakini kwenye kalori (nishati ya vyakula) zinazoingia ndani ya mwili na zinazotokanje.

MAPENDEKEZO;

Unatafuta kuunda shepu ya umbo (curve) zaidi? Zingatia mazoezi yako ya nguvu kwenye mabega yako na misuli ya chini ya mwili kama makalio na mapaja. Utaratibu wa kujenga misuli ya misuli unapendekezwa sana. Na wanawake, imesemwa hapo awali lakini inahitaji kurudiwa tena: Hauta jaa mwili wako! Badala yake, utaongeza umbo fulani lenye muenekano wa kuvutia (sexy/curved).



UNAWEZA FANYA NINI?

Kwa kuwa umegundua umbo la mwili wako na hatari inayoweza kutokea kiafya, unaweza kuchukua udhibiti zaidi wa afya yako. Lakini bila kujali una umbo la peazi au umbo la tufaha na mengine, unapaswa kuzingatia wakati wote kuwa ni mwenye afya.

  • Kula vizuri ili ujisikie vizuri. Dumisha lishe yenye usawa, yenye nyuzi nyingi, matunda,  mboga za majani , protini na kiwango cha chini katika mafuta na sukari.
  • Pendelea kufanya mazoezi! Kukaa  kwa mda mrefu huhimiza mkusanyiko wa mafuta katika tumbo. Fanya angalau kwa dakika 30 mazoezi ya wastani/nguvu mara 3-5 kwa wiki.
  • Fanya mabadiliko ya mtindo wa maisha yako. Kunywa pombe sana na uvutaji sigara kwa wingi kunaweza kusababisha mafuta hatari kujaa eneo la tumbo.

Kupenda muonekano wako ni ziada ya ziada, Afya kwanza!